×

Aunty: Kuuza Nguo Sio Umaskini

AUNTY Ezekiel Grayson Jujuman; ni mwanamama mkali kunako Bongo Movies ambaye anasema kuwa, kitendo cha kuamua kuuza nguo zake hivi karibuni haimaanishi kuwa ameishiwa au ni maskini.

 

Aunty anasema kuwa, kikubwa ni kwamba anataka mashabiki wake kushea vitu vyake na ni ishara ya kuwa nao pamoja ndiyo maana hata nguo anauza kwa bei rahisi mno.

 

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA, Aunty anasema kuwa, ameamua kufanya hivyo kwa upendo tu, lakini kinachoshangaza ni watu kusema kuwa ameishiwa au amefilisika.

 

Aunty anasema si kweli kwamba amefilisika, lakini kikubwa alitaka watu washee vitu vyake. “Kwa hiyo kama kufilisika wanavyosema, sasa ndiyo nianze kuuza nguo? Kuuza nguo zangu siyo umaskini.

 

“Kama ni kufilisika si ningeaza kuuza nyumba? Watu hawajui tu, mimi nataka kushea upendo tu kwa mashabiki wangu maana siyo rahisi kwanza mtu atoe nguo zake hata kama wanatoa pesa, lakini mimi ni upendo tu,” anasema Aunty; mama wa watoto wawili.

Leave a Comment