×

Kijiji Ambacho Wakazi Hulala Kwenye Miti Licha ya Kuwa na Nyumba

WAKAZI wa Kijiji cha Malelei, kilichopo katika Kaunti ya Lamu sasa wanalazimika kulala juu ya miti licha ya kuwa na nyumba zao kwa hofu ya kushambuliwa na wanamgambo wa kundi la kigadi la Al-Shabab.

 

Kwa mujibu ya ripoti kutoka eneo hilo zinadai kuwa, wakazi wanatumia muda wa mchana tu kuwa makwao na kufanya kazi zao za nyumbani kama vile ukulima na punde tu giza linapoingia wanakimbia kujificha kwenye miti.

 

Katika mashambulizi ya hivi maajuzi, wanamgambo wa Al-Shabaab wamekuwa wakishambulia maboma ya wakazi hao na kuwaua kikatili na waathiriwa wengi wakiwa wanaume. Visa hivyo vimeshuhudia zaidi ya watu 15 kuuawa na zaidi ya nyumba 15 kuteketezwa.

 

Mnamo Januari 10, 2022, watu wawili waliuawa na nyumba kadhaa kuteketezwa kufuatia shambulizi liliotekelezwa katika kijiji cha Salama, Kaunti ya Lamu. Wakaazi wa Juhudi, Salama na Widhu eneo la Majembeni, Kaunti ya Lamu walilazimika kukesha nje na baridi kali kufuatia majibizano makali ya risasi.

 

Wakazi wa walitoroka kutoka mboma yao na kwenda kujificha usiku huo katika shule zilizoko karibu, idadi nyingine katika soka la Kibaoni na wengine hata kukesha vichakani. Shambulizi hili linajiri siku chache tu baada ya wavamizi kumimina risasi kadhaa na kusababisha wazi wa Mejembeni kutoroka eneo hilo.

 

Katika kisa kama hicho, mnamo Januari 3, wavamizi waliokuwa wamejihami kwa silaha zikiwemo panga na bunduki, waliwauwa watu sita na kuteketeza nyumba kadhaa kabla ya kutoroka eneo la Widhu Majembeni, kaunti ya Lamu.

 

Kwa mujibu wa Kamishna wa Kaunti ya Lamu Irungu Macharia, raia mmoja aliuawa kwa kupigwa risasi, mwingine akakatwa hadi kuaga dunia huku wengine wanne wakiteketezwa wakiwa katika nyumba zao.

 

Awali, iliripotiwa kuwa shambulizi hilo lilitekelezwa na wanamgambo wa kundi la kigaidi la Al Shabaab waliosemekana kuonekana katika msitu wa Boni. Hata hivyo, Inspekta Jenerali wa Polisi Hilary Mutyambai alifafanua kuwa uchunguzi uliashiria shambulizi hilo kuchochewa na mizozo ya shamba miongoni mwa masuala mengine.

Leave a Comment