Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Frank Nyabundege (kushoto) akiongea na wafanyakazi wa benki hiyo wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika katika makao makuu ya Benki hiyo yaliyopo Dar es Salaam jana.Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Frank Nyabundege (wa pili kulia) akikata keki ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya Wanawake duniani. Waliomzunguka ni baadhi ya wafanyakazi wanawake wa benki hiyo.
Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Frank Nyabundege (kushoto) akigonganisha glasi na Afia Sigge ambaye ni kaimu mkurugenzi wa maendeleo ya biashara wa benki hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani jijini Dar es Salaam jana.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika katika makao makuu ya Benki hiyo yaliyopo Dar es Salaam jana.