×

Simba Yatangaza Kishindo Kipya Kuwavaa Rs Berkane – Video

Klabu ya Simba leo Machi 9, 2022 imeingia kambini kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa makundi kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya Rs Berkane ya Morroco kwenye mchezo unaotarajiwa kuchezwa siku ya jumapili saa kumi kamili jioni kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

 

Meneja wa habari na mawasiliano hiyo, Ahmed Ally amesema wameingia mapema kambini kwa ajili ya kuonesha umuhimu wa mchezo huo huku nyota wawili pekee ambao watakosekana kwenye mchezo huo.

“Taarifa ya awali kuhusu majeruhi ni kuwa Hassan Dilunga atakosekana kwenye mchezo na Clotas Chama anakosekana kutokana na kanuni za kimashindano ila Taddeo Lwanga, Kibu Denis, Chris Mugalu na Jonas Mkude wapo tayari kwa mchezo.

“Nawaomba mashabiki wetu tununue tiketi mapema. Wengi wetu tumekuwa na utaratibu wa kunua tiketi siku ya mchezo lakini ni jambo la kupendekeza siku ya mchezo kufika tukiwa na tiketi mkononi.”

 

“Kuna jambo lilijitokeza kwenye mchezo dhidi ya Asec la kuwaondoa mashabiki wao. Niwaombe kwenye mchezo huu tusifanye hivyo, tunaona siku ile baada ya mchezo waliondoka uwanjani kwa aibu.”

 

“Tanzania kwa sasa tupo nafasi ya 10 kwa kuwa na Ligi Kuu bora Afrika, hili halijaja pekee kwa michezo ya ndani bali kwa namna ambavyo tunafanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa ambayo tunashiriki.”

 

Berkane wamekuja wakati mbaya maana wametukuta tuko kamili.”- amesema Ahmed Ally.

Klabu ya Rs Berkane ambayo ni kinara wa kundi D inatarajiwa kuwasili kesho majira ya saa sita kamili mchana huku Simba ikikamata nafasi ya pili wakiwa na alama 4 sawa na timu ya US Gendermarie ya Niger huku Asec Mimosa ya Ivory Coast wakiwa wa mwisho na alama 3.

Leave a Comment