×

TBA Yaupiga Mwingi, Yakarabati Nyumba za Wapangaji na Viongozi – Video

UONGOZI wa Wakala wa Majengo nchini (TBA) umefanya ziara katika maeneo ambayo wanafanya ukarabati mkubwa wa majengo yakiwemo yale ya Mjini Dar es Salaam, Mikocheni na Masaki ili kujionea kazi kubwa inayofanywa kukarabati nyumba za kuishi na majengo ya viongozi.

Akizungumzia ziara hiyo, Mtendaji Mkuu wa TBA, Arch. Daud Kondoro amesema lengo kubwa ni kuhakikisha nyumba hizo zinakuwa kwenye hali nzuri, nje, rangi na mapaa pamoja na kuweka nembo za TBA kwa ajili ya utambuzi wa majengo hayo.

Mtendaji Mkuu wa TBA, Arch. Daud Kondoro akizungumzia ukarabati huo.

Haya mambo yote yamefanyika kupitia kiwanda cha TBA ambacho kipo Magomeni na ndio kinafyatua matofali yanayotumika katika ukarabati huo.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Miliki TBA, Said Mndeme amesema wamekarabati maghorofa kwa kurekebisha mifumo ya maji taka, kurekebisha rangi za wakala kwa majengo yote, kurekebisha mapaa na kudhibiti uvujaji wa maji katika mapaa ya juu (ya ghorofa) ambayo yamejengwa kwa zege.


Kwa nyumba za chini ambazo ni za zamani na zilitekelezwa kwa sababu ya uchakavu, TBA imefanya ukarabati mkubwa kwa kuzipaua, kuzipiga plasta upya na kuzifanya kuwa za kisasa. Vyumba vyote kwa sasa ni self-contained bedrooms na zina kamera na fensi, maua, paving blocks na nakshi nyingine pamoja na maeneo ya majiko na ya kufulia.


Aidha, Kondoro imeishukuru Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuipa pesa TBA ambazo zimeisaidia kufanya ukarabati huo mkubwa ambao umekuwa na manufaa makubwa.

 

Leave a Comment