
KUTOKA kwenye Ukurasa wa Instagram wa msanii nguli wa Bongo Fleva, Hamisi Baba ‘H.baba ameandika.
”Diamond Platnumz Ndio Mwanamuziki Bora Africa na sio No 3 ni No 1 ila wamekosea kiubinadamu tumewasamehe Diamond sio msanii maarufu nimwanamuziki mkubwa Africa,
Umaarufu ata mimi ni maarufu ila Diamond ni mwanamuziki mkubwa Africa na duniani tunajivunia hilo, nakujibu kama ifuatavyo kaka angu Unaesema ni maarufu tuu sio bora, kwanza ujue huyu Naseeb sio msanii.
Ni Mwanamuziki aliekamilika kuwa mwanamuziki, pia nibora kwasababu toka ameanza mziki 2009 mpaka leo 2022 ajashuka anastahili heshima kubwa, amekuwa bora mpaka leo hii ni bora tuu, walijaribu kumtikisa akutikisika, wakamuyumbisha akuyumba kasimamia misimamo yake tu.
Kafanikiwa tupunguze wivu aliekuzidi kakuzidi tuu tujifunze kupitia Diamond tumpe eshima yake kwa Hili nasimama na Diamond ndio ngao yetu watanzania kaupiga Mwingi kwenye muziki leo Wanamuziki wengine wanatembea vifua mbele.
Bila Diamond wasingethubutu, Kiukweli Damond anastahili eshima kubwa saaana Kuongea kupo ila ukweli unatuumiza wengi, mimi leo nalipwa kwa show moja Mil. 10 mpaka Mil. 15 kwasababu ya Diamond.
Tulikuwa tunalipwa laki 3 mpaka m.1 mwisho muulizeni Babu Tale nishapambana nae sana kwenye show hizo yupo na tip top yake, tuondoe chuki Shikamoo Diamond umetufanya tueshimike tukiwa nje ya Tanzania.
Kuna wanamuziki leo hii wanalipwa m.70 ndani nje mpaka M.100 kwa show moja tuu yoote hiyo ni @diamondplatnumz kwangu Simba nibora zaidi yao, leo nimetoa #EP. DUKUDUKU kwasababu ya #EP ya (FOA) yake @diamondplatnumz.
Nimesikiliza katisha kinoma #EP nyimbo 10 zoote kali kinoma, Namimi nikapata nguvu kupitia SIMBA sio SISIMIZI SIMBAAAA AAA Nimetoa #EP yangu.
LINK IN MY BIO 👆 #EP DUKUDUKU Inapatikana platform zoote nipo….
Onyo: @diamondplatnumz Usipost #EP yangu ya #DUKUDUKU watakufa wengi kausha hivyo hivyo
TANGAZO: NIPO *TIK TOK* OFFICIAL_H.BABA” @h.baba_
KUSIKILIZA #FOA EP INGIA HAPA ==> #FOAtheEP