×

Msanii Kanye West Afungiwa Instagram Kwa Saa 24

Kanye West amepigwa marufuku kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram kwa saa 24 baada ya kutumia lugha ya kibaguzi dhidi ya mchekeshaji maarufu, Trevor Noah.

 

Rapa huyo alimshambulia Trevor Noah mtandaoni baada ya msanii huyo kusema kitendo cha Kanye dhidi ya mtalaka wake Kim Kardashian ni cha ‘kutisha’.

 

Kanye amekosolewa kwa kuwaangazia mara kwa mara Kim, watoto wao na mpenzi wake Pete Davidson mtandaoni.

Meta, ambayo inamiliki Instagram, ilisema rapa huyo alikiuka sera za jukwaa hilo kuhusu matamshi ya chuki na uonevu.

 

Kampuni hiyo pia ilisema sera zake kuhusu unyanyasaji zimekiukwa.

Ingawa akaunti yake bado inaonekana, Kanye hawezi kuchapisha chochote kwenye mtandao huo, kutoa maoni au kutuma ujumbe wa moja kwa moja.

 

Katika machapisho ya hivi karibuni, Kanye amemshutumu Kim kwa kumzuia kuona watoto wao – jambo ambalo amekanusha.

Katika taarifa, Meta ilisema itachukua ‘hatua za ziada’ ikiona ukiukaji zaidi wa sera zake.

 

“Mara nyingi tunachukua hatua za ziada dhidi ya akaunti ambazo zinavunja sheria mara kwa mara kwa kuweka vikwazo kwenye akaunti zao,” ilisema taarifa hiyo.

 

Meta iliongeza kuwa pia ‘imefuta maudhui’ kutoka kwa akaunti ya Kanye.

Trevor Noah alitoa maoni hayo wakati wa kipindi cha habari za kejeli anazoandaa, The Daily Show.

PRODUCER wa HARMONIZE Afunguka KUHUSU EP ya DIAMOND | BONGO 255…

Leave a Comment