×

Rais Samia Azindua Mradi Wa Maji Mlandizi Chalinze – Video

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Chalinze mkoani Pwani katika Mkutano uliofanyika Viwanja vya Polisi Chalinze Mkoani Pwani mara baada ya kuzindua mradi wa maji wa Mlandizi-Chalinze-Mboga leo tarehe 22 Machi, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, ameeleza kufurahishwa na kukamilika kwa mradi wa Maji wa Chalinze ambao utahudumia wananchi takribani laki mbili.

Amesema hayo leo Machi 22, 2022 ambayo ni siku ya Maji Duniani huku akiweka wazi kuwa yeye mwenyewe wakati wa Kampeni alifika Chalinze na akajionea taabu ya maji waliyokuwa wakipata wananchi.

Wananchi wa mkoa wa Pwani wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokua akizungumza nao kwenye Mkutano baada ya kuzindua mradi wa maji wa Mlandizi-Chalinze-Mboga katika tukio lililofanyika Chalinze mkoani Pwani leo tarehe 22 Machi, 2022.

”Nakumbuka nilimuona mwanangu Ridhiwani akifoka moto mdomoni unatoka akimfokea Eng. Cyprian Luhemeja, akimwambia usipoleta maji hapa nakushtaki kwa wananchi lakini leo nimeona kila mmoja kamuomba radhi mwenziwe baada ya maji kupatika Chalinze” – Rais Samia Suluhu.

 

Aidha kwa upande mwingine, Rais Samia amesema Serikali yake itatoa shilingi Bilioni 1 kwa awamu mbili kwaajili ya kusambaza maji kwa wananchi wa Pwani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiondoa Kitambaa kuzindua mradi wa maji wa Mlandizi-Chalinze-Mboga katika tukio lililofanyika Chalinze mkoani Pwani leo tarehe 22 Machi 2022.

”Kwakweli kazi kubwa imefanyika hapa Pwani. Kazi iliyobaki ni kusambaza kwa wananchi. Nitawapa DAWASA Mil 500, tutaangalia kasi yenu ikiwa nzuri tunaongeza 500, lakini hii pesa mtakuja kuirudisha kwenye mfuko niliotoa kwasababu wananchi watawalipa” – Rais Samia Suluhu.

 

⚫️ SIKILIZA + 255 GLOBAL RADIO LIVE: http://ndstream.net/globalradio/ ⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

 

Leave a Comment