×

Jeshi Lazingira Makazi ya Makamu wa Rais

VIKOSI  vya serikali ya Sudan Kusini vimeripotiwa kuzingira makazi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Riek Machar katika mji mkuu Juba.

 

Hatua hiyo inajiri siku moja tu baada ya kiongozi huyo wa zamani wa waasi kuwataka viongozi wa kikanda na kimataifa kuingilia kati kumaliza mapigano mapya katika majimbo ya Unity na Upper Nile – ambayo yanachukuliwa kuwa ni ngome zake.

 

Kwa wiki kadhaa sasa, mapigano kati ya jeshi la Sudan Kusini na vikosi tiifu kwa Bw. Machar vimeripotiwa katika maeneo mbalimbali, na kutishia makubaliano tete ya amani kati yake na Rais Salva Kiir.

 

Serikali haijatoa tamko lolote kuhusu iwapo wanajeshi wake wamezingira majengo hayo haijulikani iwapo  Machar yuko katika nyumba hiyo ama la.

Leave a Comment