×

Ukraine: Putin Anapotoshwa na Washauri Wake Waoga Vita vya Ukraine

Rais wa Urusi Vladimir Putin.

Rais wa Urusi Vladimir Putin anapotoshwa na washauri ambao wanaogopa sana kumwambia jinsi vita vya Ukraine vinavyoendelea vibaya, Ikulu ya Marekani inasema.

Wakati huo huo idara ya kijasusi ya Uingereza inasema kuwa wanajeshi wa Urusi nchini Ukraine wamekatishwa tamaa, hawana vifaa na wanakataa kutekeleza maagizo.

 

Bw.Putin pia haambiwi kuhusu athari kamili ya vikwazo kwa uchumi wa Urusi, Ikulu ya Marekani ilisema.

Kremlin bado haijatoa maoni juu ya tathmini hizo.

 

Msemaji wa Ikulu ya White House, Kate Bedingfield alisema Marekani ilikuwa na habari kwamba Bw Putin “alihisi kupotoshwa na jeshi la Urusi” na hii imesababisha “mvutano unaoendelea kati ya Putin na uongozi wake wa kijeshi”.

 

“Vita vya Putin vimekuwa kosa la kimkakati ambalo limeiacha Urusi kuwa dhaifu kwa muda mrefu na kuzidi kutengwa katika ulimwengu,” alisema.

 

Msemaji wa Pentagon John Kirby amesema kuwa Putin ambaye hana taarifa za kweli anaweza kusababisha juhudi” katika kumaliza mzozo kupitia mazungumzo ya amani kutozaa matunda.

“Nyingine ni kwamba, hujui kiongozi wa namna hiyo atapokeaje habari mbaya,” alisema.

SIMBA Yatenga MIL 800 Kuwamaliza GENDERMARIE, Huku YANGA Wamvuta STAA wa STARS | KROSI DONGO

Leave a Comment