×

Rais Samia Afanya Mabadiliko Madogo ya Baraza la Mawaziri

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Samia Suluhu Hassan leo Machi 31, amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri kama ifuatavyo

 

George Boniface Simbachawene, !Waziri wa Katiba  na Sheria, amehamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera  na  Uratibu

 

Damasi Daniel Ndumbaro, Waziri wa Maliasili na Utalii amehamishiwa Wizara ya Katiba na Sheria kuwa Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria.

 

Pindi Hazara Chana , Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge, Sera na Uratibu) amehamishiwa Wizara ya Maliasili na Utalii kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii.

 

Leave a Comment