
KLABU ya Soka ya Simba SC imepangwa kukutana na Klabu ya Orlando Pirates ya nchini Afrika Kusini katika hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Simba ilifanikiwa kutinga katika hatua hiyo baada ya kuichakaza Klabu ya US Gendarmerie jumla ya mabao 4-0 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Simba ilimaliza katika nafasi ya pili kwenye kundi D na sasa kwa mujibu wa ratiba mechi yake ya kwanza itaanzia nyumbani April 17 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa na kumalizia mechi ya marudiano Aprili 24 nchini Afrika Kusini.
Droo hiyo iliyochezeshwa nchini Misri itawakutanisha Simba na Orlando Pirates ambao walimaliza hatua ya makundi wakiwa na jumla ya pointi 13 katika kundi C