×

Rais Samia: Serikali Kumwaga Magari ya Wagonjwa 258 Nchi Nzima

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akibonyeza Kitufe kuzindua Mfumo wa usafirishaji wa dharura kwa wajawazito na watoto wachanga (M-MAMA) katika hafla iliyofanyika Viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma leo tarehe 06 Aprili, 2022.

RAIS  Samia Suluhu Hassan amesema magari ya wagonjwa 233 ya kawaida yanatarajiwa kumwagwa Tanzania nzima, huku mengine 25 zenye hadhi ya rufaa pia yakitarajiwa kuwasili.

 

Rais Samia ameyasema hayo leo Aprili 6, 2022 katika uzinduzi wa mfumo wa usafirishaji wa dharula kwa wanawake wajawazito na watoto wachanga (M-MAMA) unaotekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na kampuni ya Vodacom.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkurugenzi wa M-MAMA Bi. Dolorosa Duncan kuhusu Mfumo wa usafirishaji wa dharura kwa Wajawazito na Watoto wachanga (M-MAMA) kabla ya kuuzindua katika hafla iliyofanyika Viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma leo tarehe 06 Aprili, 2022.

Rais Samia amesema pamoja na jitihada zote zinazofanywa na Serikali lakini pia imejithidi kuhakikisha kuwa walau kila kata inakuwa na gari moja la wagonjwa.

 

“Tumeagiza ambulance 233 za kawaida ambazo zitamwagwa Tanzania nzima lakini pia tumeagiza ambulance 25 kama ngazi ya rufaa ile ya kawaida ikiwa haitoshi haina vifaa basi hizo ni zitatumika maana zinafanana na kituo cha afya ngazi ya kata,” amesema Samia.

Viongozi mbalimbali pamoja na wananchi wa Mkoa wa Dodoma wakiwa katika viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma kuhudhuria hafla ya uzinduzi wa Mfumo wa usafirishaji wa dharura kwa Wajawazito na Watoto wachanga (M-MAMA) uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan leo tarehe 06 Aprili, 2022.

Amesema pia wameagiza magari 242 za uratibu huku akieleza kuwa ni matumaini yake kuwa zitakwenda kuongeza nguvu katika mpango wa M-mama ili kuwawahisha watoto na kinamama hospitalini.

Amesema kukamilika kwa anuani za makazi pia kutasaidia kuweka urahisi wa uchukuaji wa wagonjwa kwenye maeneo yao kwenda hospitalini kutokana na urahisi katika kuelekeza.

Leave a Comment