×

NBC leo Yazindua Kampeni ya ‘Jaza Kibubu na NBC’

Mkuu wa Bidhaa na Mauzo wa Benki ya NBC, Abel Kaseko (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari   jijini Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Jaza Kibubu Tusepe kuwa wateja 80  wa benki hiyo watashinda tiketi za kushuhudia mchezo wa watani wa Jadi Simba na Yanga utakaochezwa kwenye Uwanja cha Mkapa jijini Dar es Salaam kulia ni Meneja Mauzo wa NBC, Deogratius Kibodya na katikati ni meneja bidhaa na mauzo, Dorothea Mabonye.
Benki ya Taifa ya Biashara NBC leo imezindua Kampeni ya ‘Jaza Kibubu na NBC’  yenye lengo la kuweza kutoa elimu kwa watanzania wote kuhusu utunzaji fedha katika sehemu salama
ambapo Kampeni hiyo itamnufaisha mtumiaji wa Account ya NBC kwenda kushiriki kutazama Live kombe la Dunia nchini Qatar na Mechi dhidi ya Simba na Yanga uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mauzo na Masoko Abel Kaseko alisema mteja atakayehitaji kushiriki Kampeni hiyo atembelee tawi la NBC au Wakala yeyote akiwa na kitambulisho Cha NIDA ambapo mteja atafunguliwa account na kuongeza kuwa Kampeni hiyo itakuwa na zawadi mbalimbali ambazo zitamfanya mteja kwenda kushuhudia mechi ndani na nje ya nchi;

 

“Kampeni hii ya jaza kibubu na NBC itakuwa na zawadi ambazo zitawawezesha wapenzi wa Mpira kuweza kuhudhuria mechi ya Simba na yanga ambayo itafanyika tarehe 30/4/2022 ambapo sisi kama NBC tutagharamikia safari, maladhi, chakula na vinywaji kwa watu 50 kutoka mikoani na wapenzi wa mpira waliopo Dar es salaam tutawazawadia watu 50 pia kuhudhuria mechi hiyo pia na wote watapewa tiketi ya VIP, na zawadi hiyo itatoka mwezi huu wa nne”

Hafla ikiendelea.

Aidha Abel alisema mbali na Mechi ya Simba na Yanga kutakuwa na mashindano ya kombe la Dunia ambayo yatafanyika nchini Qatar ambapo wao kama Benki ya NBC watagharamikia vitu mbalimbali kwa mteja ambaye atajishindia kwenda kushiriki kutazama mechi hiyo;

“Tunatambua kuwa mwaka huu kutakua na mashindano ya kombe la Dunia ambayo yanafanyika Qatar mwezi November Hadi Desemba 2022 sisi kama Benki ya NBC tutatoa tiketi 5 kwa watanzania ambao ni wapenzi wa mpira kwenda kushuhudia kombe la Dunia na tiketi zote ambazo tutatoa ni VIP, mbali na tiketi pia tutagharamikia safari kwa watu wote kutoka Dar es Salaam hadi Qatar ambapo tutagharamikia maladhi, chakula na vinywaji lakini pia tutatoa posho kwa watu ambao wataenda kuhudhuria mechi hizo ambazo pia ni tiketi za VIP”

 

Mbali na hayo Menenja Masoko huyo alisema Kampeni hiyo iliyozinduliwa leo itaendeshwa kwa ndani ya miezi Sita na mshindi wa kwenda Qatar atapatikana mwezi September 2022

Naye Meneja Mauzo na Biashara upande wa Wateja Binafsi, Dorothea Mabonye alifafanua Jinsi ya mteja atakavyoweza kujishindia safari ya kwena Qatar ambapo mteja anatakiwa kuweka fedha kuanzia Milioni 7;

 

“Jinsi ya kufanya ili ushinde safari ya Qatar unatakiwa uweke fedha kuanzia Milioni Saba na kuendelea lakini Milioni Saba hii unaiweka kidogokidogo mpaka mwezi wa Tisa na ndipo utapata nafasi ya kuingia kwenye droo na uwe mmoja ya wale ambao watakaokwenda Qatar kuangalia live kombe la dunia”

Aliongeza kuwa kwa mteja ambae ataweka Milioni 10 na kuendelea kidogokidogo atapata nafasi ya kupata tiketi ya  VIP hivyo kutakua na wateja watano ambapo wawili watakua ni wa VIP na watatu watakua wa tiketi za kawaida.

 

Mbali na hayo Doroth alisema wao kama wadhamini Wakuu wa ligi kuu Tanzania Bara hawajaishia tu kuwapeleka watanzaia Qatar kuangalia kombe la Dunia vilevile wanakwenda kuwazawadia watanzania wote au wateja wa NBC ambao wataweka fedha kuanzia tarehe 6 mpaka tarehe 24/4 mwaka huu kwenda kuangalia mechi ya watani wa jadi Simba na yanga ambao wanatarajia kucheza tarehe 30/4/2022 uwanja wa Taifa.

Alisema kutakuwa na jumla ya washindi 80 ambapo washindi 50 watatokea mkoani na 30 watatokea Dar es Salaam ambao wote watagharamikiwa;

“Tutakuwa na washindi 80 kwa ujumla ambapo washindi 50 watatokea mikoani nje ya dar es salaam na washindi 30 watatokea hapa dar es salaam ambapo washindi 50 tutawagharamikia usafiri kutoka walipo hadi kufika dar es salaam, malazi na chakula na kutoka hotelini mpaka uwanjani kwenda kuangalia mpira, na washindi 30 ambao  tutawapata kutoka Dar es salaam tutawapatia tiketi za VIP kuangalia mechi hiyo”

Kampeni hii ya ‘Jaza Kibubu na NBC’ ni maalum kwaajili ya watenja wa NBC, Wateja binafsi na watanzania wote ambao wangependa kufungua account ya NBC

Leave a Comment