×

Manchester City Waendelea Kung’ang’ania Kileleni mwa Msimamo wa EPL

                      Mshambuliaji wa Manchester City Gabriel Jesus akifunga goli dhidi ya Liverpool

BADO Manchester City ni vinara wa Ligi Kuu England wakiwa wametofautiana pointi moja na wapinzani wao Liverpool.

 

Zote zimecheza jumla ya mechi 31 ndani ya Ligi Kuu England msimu wa 2021/22 ambao ushindani wake ni mkubwa.

                            Sadio Mane na Kyle Walker wakiwa katika majukumu yao

Ni pointi 74 zipo kibindoni huku Liverpool wakiwa na pointi 73 kibindoni na ni mechi 22 wameshinda Liverpool huku City ambao ni mabingwa watetezi wakiwa wameshinda mechi 23.

 

Mchezo wa jana Aprili 10 uliochezwa Uwanja wa Etihad walitoshana nguvu kwa kufungana mabao 2-2 na kutoshana pointi mojamoja.

 

Mabao ya Kevin De Bruyne dk 5 na Gabriel Jesus ilikuwa dk 37 huku kwa Liverpool ikiwa no Diogo Jota dk 13 na Sadio Mane dk 46.

Leave a Comment