×

Chongolo Amtembelea Masoud Kipanya, Ajionea Gari Lake..

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo akisaini kitabu cha wageni katika Karakana ya Kaypee Motors ya Ali Masoud ‘Kipanya’ iliyopo katika eneo la Shirika la Viwanda Vidogovidogo (SIDO) Vingunguti, jijini Dar Es Salaam ambapo alifika hapo kutembelea na kujionea gari inayotumia nguvu za umeme, iliyobuniwa na Kipanya, ikiwa gari ya kwanza ya aina hiyo kubuniwa na Mtanzania.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo, ametoa siku saba kwa Shirika la Viwango Tanzania (TBS),  kufika katika kiwanda cha uzalishaji magari cha Alli Masoud maarufu Masoud Kipanya ili kufanya ukaguzi na kutoa vibali vinavyohitajika ili kuruhusu uzalishaji.
Akiwa katika ziara kiwandani hapo ameahidi ndani ya siku 14 atarudi akiwa na taasisi zote zinazohusika na udhibiti wa ubora, ili kuharakisha mchakato wa kiwanda hicho kuendelea.
Chongolo akizungumza na Ali Masoud ‘Kipanya’ (kulia) mara baada ya kutembelea karakana yake ya Kaypee Motors iliyopo eneo la Shirika la Viwanda Vidogovidogo (SIDO) Vingunguti, jijini Dar Es Salaam
Akizungumza leo tarehe 12 Aprili, 2022 Vingunguti jijini Dar es Salaam alipotembelea katika kiwanda hicho Katibu Mkuu amefafanua kuwa,
Ilani ya CCM iliahidi na imeendelea kuweka msukumo katika ubunifu, hivyo akiwa Mtendaji Mkuu wa Chama atahakikisha wanathamini mchango wa wazalishaji wa ndani kikiwemo kiwanda hicho, hivyo uwezeshaji wa kiwanda ni muhimu ili kuongeza ajira kwa wananchi, kukuza teknolojia  na kupunguza matumizi ya fedha za kigeni.

Leave a Comment