The House of Favourite Newspapers

Shilole angusha pati ya kufunga mwaka

0

 

IMG_8589Shilole (katikati) akiwa amezungukwa na baadhi ya marafiki zake.

IMG_8307Shilole akicheza muziki huku baunsa wake akimshuhudia.

IMG_8312Baadhi ya warembo waliohudhuria pati hiyo wakiwa wamepozi.

SHILOLE (3) SHILOLE (4)Sehemu ya  vinywaji  na vitoweo vilivyokuwa vimeandaliwa na Shilole kwa ajili ya kuhakikisha anatimiza azma yake ya kufurahia na kusherekea   siku chache za kufunga mwaka 2015 na baadhi ya wasanii na marafiki zake waliojitokeza mahali hapo,usiku wa kuamkia leo.

SHILOLE (5) SHILOLE (6)Waalikwa wakibadilishana mawazo kwa pozi tofauti.

SHILOLE (7)Baadhi ya marafiki zake wakibadilishana mawazo huku wakinywa supu iliyokuwa maalum kwa ajili ya sherehe hiyo.SHILOLE (8)Sehemu ya waalikwa waliohudhuria mahali hapo.SHILOLE (10) SHILOLE (11)Warembo wakiwa kwenye pozi la pamoja wakati wa sherehe hiyo.SHILOLE (12) SHILOLE (13)Baadhi ya marafiki waliojitokeza kusherehekea pamoja na Shilole.

Habari/Picha: Musa Mateja

STAA anayewakilisha kwenye tasnia ya filamu na Bongo Fleva, Zuwena Mohame ‘Shilole’, usiku wa kuamkia leo ameangusha bonge la pati la nyumbani  kwake Kijitonyama jijini Dar es Salaam, ambapo aliteketeza kiasi cha sh.  mil. 3, kwa kununua mbuzi wanne na kuku zaidi ya 50, huku vinywaji vya kila aina vikitawala pati hiyo kiasi cha kuwafanya waalikwa kunywa hadi kusaza.

Akizungumzia maandalizi hayo Shilole alisema kwamba, pati hiyo ina maana ya kujipongeza kutokana na misukosuko mbalimbali aliyoipata kwa muda wa mwaka mzima, mbali na hivyo, Shilole alisema kwamba, ameamua kuandaa vitu vyote ili apate muda wa kubadilishana mawazo na baadhi ya wasanii na marafiki zake ambao amekuwa akishirikiana nao kwa mambo mengi katika harakati zake za kusaka mkate wa kila siku.

“Nimeamua kuandaa pati hii kwa lengo la kutaka kukaa na wasanii na marafiki zangu ili tuweze kubadilishana mawazo, lakini mbali na hivyo pia nimeamua kusherehekea kutokana kwamba tunaelekea kwenda kufunga mwaka ambapo nimepitia mihangaiko mikubwa kwenye familia yangu na leo naona kama mambo yanaanza kunyooka baada ya mambo fulanifulani kuachana nayo,” alisema Shilole.

Leave A Reply