
Meli ya Urusi ya kusafirisha makombora imezama katika “bahari yenye dhoruba” wakati ikivutwa baada ya kutokea mlipuko wa risasi ulioathiri sehemu ya meli hiyo, wizara ya ulinzi ya Urusi imesema katika taarifa yake.
“Meli ya Moskva ilipoteza uthabiti ilipovutwa hadi bandarini kwa sababu ya uharibifu wa sehemu ya meli ambao ulitokea kutokana na mlipuko wa moto wa risasi. Katokana na hali ya dhoruba ya bahari, meli imezama,” gazeti la The Guardian la Uingereza limeripoti likunukuu taarifa ya Wizara ya Ulinzi ya Urusi.
Urusi na Ukraine zimetoa maelezo yanayokinzana kuhusu kilichotokea kwenye meli hiyo. Ukraine ilidai meli hiyo ilipigwa makombora ya Neptune wakati Urusi ikisema moto uliotokea kwenye meli hiyo nakusababisha risasi kulipuka.

Meli hiyo ya kubeba makombora na wafanyakazi 510 ilikuwa ishara ya nguvu za kijeshi za Urusi, ikiongoza mashambulizi yake ya majini dhidi ya Ukraine.
Kyiv inasema makombora yake yaligonga meli hiyo ya kivita. Moscow haijaripoti shambulio lolote. Inasema chombo kilizama baada ya moto.
Moto huo ulisababisha mlipuko wa risasi za meli hiyo ya kivita, Urusi inasema, na kuongeza kuwa wafanyakazi wote baadaye walihamishwa hadi kwenye meli za karibu za Urusi katika Bahari Nyeusi. Haikutoa maelezo zaidi.
Baada ya kusema awali meli ya kivita ilikuwa inaelea, Alhamisi jioni vyombo vya habari vya serikali ya Urusi vilitangaza habari kwamba Moskva ilikuwa imepotea.
“Wakati wakivutwa… kuelekea bandari iliyokusudiwa, meli hiyo ilipoteza usawa wake kutokana na uharibifu uliokuwa ndani ya meli wakati moto ulipozuka baada ya risasi kulipuka. Kutokana na hali ya bahari iliyochafuka, meli hiyo ilizama,” shirika la habari la serikali Tass lilinukuu Wizara ya Ulinzi ya Urusi.
Maafisa wa kijeshi wa Ukraine walisema waliipiga Moskva kwa makombora ya Neptune yaliyotengenezwa na Ukraine – silaha iliyoundwa baada ya Urusi kutwaa eneo la Crimea mwaka 2014, na tishio la majini kwa Ukraine katika Bahari Nyeusi liliongezeka.
Afisa mkuu wa Ukraine alisema kuwa wafanyakazi 510 wangeweza kuwa ndani ya Moskva.
Katika siku ya kwanza ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine tarehe 24 Februari, Moskva ilipata sifa mbaya baada ya kukitaka kikosi kidogo cha askari wa mpaka wa Kiukreni wanaotetea Kisiwa cha Snake katika Bahari Nyeusi kujisalimisha – ambapo kwa kumbukumbu walitangaza ujumbe wa kukataa.
Meli hiyo ilijengwa katika enzi ya Soviet, Moskva iliingia huduma mapema miaka ya 1980. Meli hiyo iliwekwa chini katika mji wa kusini mwa Ukraine wa Mykolaiv, ambao umeshambuliwa kwa bomu na Urusi katika siku za hivi karibuni.
Meli hiyo ya kusafirisha makombora hapo awali ilitumiwa na Moscow katika mzozo wa Syria ambapo ilivipa vikosi vya Urusi nchini humo ulinzi wa majini.
Inaripotiwa kuwa ilikuwa na makombora 16 ya kuzuia meli ya Vulkan na safu ya silaha za kupambana na manowari pamoja na topedo.
Ikiwa shambulio la Ukraine litathibitishwa, Moskva yenye tani 12,490 itakuwa meli kubwa zaidi ya kivita kuzamishwa na hatua ya adui tangu Vita vya Pili vya Dunia.
Ni meli ya pili kubwa ambayo Urusi imepoteza tangu kuanza kwa uvamizi wake. Mnamo Machi, meli ya kutua ya Saratov iliharibiwa na shambulio la Ukraine katika bandari ya Berdyansk, Bahari ya Azov ya Kiukreni ilitekwa na Urusi.