
Urusi imesema kuwa itahakikisha kunakuwa na usalama wa maisha ya wanajeshi wa Ukraine katika Mariupol wanaojisalimisha watakaojisalimisha katika kipindi cha saa kadhaa zijazo.
Kuanzia saa kumi na mbili za Urusi au saa tisa alasiri kwa saa za Afrika mashariki, na baada ya hapo vikosi vya Urusi vimesema vitawaruhusu wanajeshi kuondoka kutoka katika eneo lenye viwanda vya chuma la Azovstal – ili mradi waache silaha zao na zana nyinginezo za kijeshi nyuma.
Wale ambao watafanya hivyo watatendewa kulingana na mkataba wa Geneva kuhusu wafungwa wavita, taarifa kutoka Wizara ya ulinzi ilisema.

Taarifa iliyotolewa saa kadhaa zilizopita imekuwa ikitangazwa kwa kina maelezo ya mkataba kwa wanajeshi wa Ukraine kila baada ya dakika 30 usiku mzima.
Kama watakubali, Urusi inasema, vikosi vya Urusivitapandisha bendera nyekundu saa kumi na mbili alfajiri na Ukraine inapaswa kupandisha bendera nyeupe kuzingira ukuta wote wa kiwanda cha chuma.
Maafisa wa Ukraine hawajatoa ishara yoyote kwamba wanapanga kukubali ofay a kuondoka eneo hilo wala kujisalimisha.
“Wanajeshi wetu wamezingirwa, majeruhi wamezingirwa. Kuna hali mbaya ya kibinaadamu… Licha ya hayo, vijana wetu wanajilinda.” amesema Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy
Maelezo yaZelenskyyyanalingana na yale ya Urusi kwamba wapiganaji wote wa mwisho wa Ukraine katika mji wa Mariupol wamezingirwa katika majengo ya kiwanda cha kufua chuma cha Azovstal.
Zelenskyy alisema amezungumza kwa njia ya simu na viongozi wa Uingereza na Sweden kuhusu hali kwenye mji wa Mariupol anayosema kuwa ya hatari na kwamba Urusi inajaribu kumuangamiza kila mtu kwenye eneo hilo.
Madai ya Moscow kwamba ilishachukuwa udhibiti kamili wa mji wa Mairupol, eneo ambalo limeshuhudia mapigano makali na hali mbaya kabisa ya kibinaadamu, hazikuweza kuthibitishwa na vyanzo huru.
Endapo Mariupol itatekwa, utakuwa mji wa kwanza kuangukia mikononi mwa vikosi vya Urusi tangu ianzishe uvamizi wake Februari 24.