
KLABU ya Chelseas imefanikiwa kutinga Fainali ya Kombe la FA baada ya kuifunga Crystal Palace kwa jumla ya mabao 2-0.
Kwenye mchezo ambao ulipigwa katika Uwanja wa Taifa wa Uingereza maarufu kwama Wembley ulishuhudiwa mabao ya Ruben Loftus Cheek pamoja na Mason Mount ambao wote ni vijana waliokulia katika kituo cha kulelea vijana cha Klabu hiyo (Academy).

Kutokana na matokeo hayo sasa Chelsea ataungana na Liverpool katika hatua ya fainali baada ya hapo juu Liverpool kuifunga Manchester City kwa jumla ya mabao 3-2.
Chelsea atakutana na Liverpool akiwa na kumbukumbu ya kupoteza kombe la Capital One mikononi mwao kwa mikwaju ya penati mapema mwezi Machi.