×

Mwanaume Nchini Marekani Afariki kwa Kung’atwa na Nyoka Aliowafuga Mwenyewe

                     Polisi wa eneo la Charles County wakichukua mabaki ya nyoka waliokuwa wamefugwa

MWANAUME aliyetambulika kwa jina la David Riston (49), mkazi wa Maryland nchini Marekani, amekufa baada ya kung’atwa na nyoka aliokuwa anawafuga ambapo maafisa wa wanyama pori wamekuta nyoka 124 wa aina mbalimbali ndani ya nyumba ya mwanaume huyo baada ya kifo chake.

 

Uchunguzi wa mwili wake umeonesha kwamba alikufa kutokana na kung’atwa na nyoka ambapo mwili wake uligunduliwa siku kadhaa baadaye na polisi baada ya kupokea taarifa kwa majirani waliodai kwamba hawamuoni Ritson akiingia wala kutoka nyumbani kwake, jambo ambalo halikuwa kawaida yake.

 

Polisi wa eneo la Charles County wameeleza kwamba baada ya kupokea taarifa kutoka kwa majirani, walifika kwenye nyumba hiyo kufanya uchunguzi ambapo walimkuta mwanaume huyo akiwa amelala sakafuni, akiwa amepoteza maisha.

 

                                         Marehemu alifuga nyoka zaidi ya 124

“Tulipofanya upekuzi ndani ya nyumba hiyo, tulikuta nyoka zaidi ya 100, wakubwa kwa wadogo, wenye sumu na wasio na sumu wakiwa kwenye tanki lililokuwa limetengezwa vizuri kwa ajili ya kazi hiyo.

 

Shirika la Habari la NBC limeripoti kuwa nyoka wenye sumu kali na hatari ambao hawaruhusiwi kufugwa walikutwa ndani ya nyumba ya mwanaume huyo, wakiwemo nyoka wakubwa aina ya chatu wa Burmese, cobra, black mamba na wengine wengi ambao idadi yao ilikuwa 124.

Leave a Comment