×

Macron Amshinda Le Pen Kiti cha Urais, Aapa Kuiunganisha Ufaransa Iliyogawanyika

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameshinda uchaguzi kwa 58.55% dhidi ya 41.45%.

Emmanuel Macron ameshinda kiti cha urais atakachohudumu kwa miaka mitano zaidi akiwa rais wa Ufaransa baada ya ushindi mnono dhidi ya mpinzani wake Marine Le Pen, ambaye hata hivyo alipata mgao wa juu kabisa wa kura za mrengo wa kulia.

 

Alishinda kwa 58.55% dhidi ya 41.45%, tofauti kubwa kuliko ilivyotarajiwa.

Kiongozi huyo aliwaambia wafuasi waliokuwa na furaha chini ya Mnara wa Eiffel kwamba sasa uchaguzi umekwisha atakuwa Rais wa wote.

 

Ndiye rais wa kwanza aliye madarakani katika kipindi cha miaka 20 kuchaguliwa tena.

Licha ya kupoteza kwake, Bi Le Pen (53), alisema sehemu yake ya kura bado ilionesha ushindi.

Leave a Comment