×

Mastaa Simba Waipania Yanga Baada ya Kushindwa Kufuzu Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho

Wachezaji wa timu ya Simba wakifanya mazoezi.

NAHODHA Msaidizi na Beki wa Kushoto wa Simba, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ amesema haikuwa bahati kwao kufuzu hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, ambapo sasa nguvu zao zote wamezielekeza katika mechi za Ligi Kuu Bara.

 

Simba imeondolewa hatua ya robo fainali ya michuano hiyo na Orlando Pirates kwa penalti 4-3, mchezo uliochezwa juzi Jumapili nchini Afrika Kusini.

 

Mchezo huo ulifikia hatua ya penalti baada ya timu hizo zote kila moja kutumia vema uwanjani kwa kupata ushindi wa bao 1-0.

 

Jumamosi hii, Simba itakuwa mgeni wa Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Tshabalala alisema: “Nianze kwa kuwashukuru benchi la ufundi, viongozi na mashabiki waliofika kwenye Uwanja wa Orlando Pirates hapa Afrika Kusini kwa ajili ya kutusapoti.

 

“Pia niwashukuru mashabiki waliokuwepo nyumbani Tanzania ambao walikuwa wakituombea tushinde mchezo huu wa marudiano dhidi ya Pirates.

 

“Kikubwa tuwaambie kuwa haikuwa bahati yetu kufuzu hatua ya nusu na badala yake tuishie hapa hatua ya robo, hivyo tunarejea nyumbani kumalizia michezo ya ligi ambayo ni muhimu kupata ushindi. Tutapambana hadi kieleweke.”

 

Simba ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, imecheza mechi 19 za ligi hiyo, inashika nafasi ya pili kwenye msimamo ikikusanya pointi 41, nyuma ya Yanga inayoongoza kwa pointi 54 baada ya mechi 20.

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza, Simba na Yanga zilishindwa kufungana.

STORI NA WILBERT MOLANDI | CHAMPIONI

Leave a Comment