Internet Society na Wadau Walivyojadili Changamoto za Kodi za Kidigitali
SHIRIKA la Internet Society Tanzania na wadau wake wamefanya workshop ya kujadili changamoto mbalimbali zilizomo kwenye mfumo mpya wa kodi za kidigitali.
Workshop hiyo iliyohusisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi imefanyika Hoteli ya Holiday Inn iliyopo Posta jijini Dar.
Akifungua mkutano huo, Mkurugenzi Mkuu Shirika la Internet Society Tanzania, Nazar Nicholas Kirama amesema ili malengo ya jambo lolote yaweze kufikia wadau wanatakiwa kuungana na kufanya kazi kwa ushirikiano kama nyuki wafanyavyo wakati wa kutengeza asali.
Rais huyo amewataka wadau hao kulijadili kwa pamoja suala hilo linaloonekana kuwa na changamoto kadhaa. Wadau hao walijadili changamoto hizo ikiwemo faida, hasara za mfumo huo mpya hapa nchini.
Wadau katika picha ya pamoja. HABARI/PICHA NA RICHARD BUKOS /GPL