
Rais wa Urusi Vladimir Putin ameonya kuwa nchi zozote zinazoingilia Ukraine zitakabiliwa na jibu la haraka.
“Ikiwa mtu kutoka nje atajaribu kuingilia Ukraine,” alisema akizungumza hivi sasa na wabunge wa Urusi, jibu letu litakuwa haraka sana.”
“Tuna zana zote za kujibu ambazo hakuna mtu anayeweza kujivunia na hatutakuwa na majisifu juu yao, tutatumia ikiwa ni lazima,” alisema.
Kiongozi huyo wa Urusi aliongeza kwamba aina ya maamuzi juu ya majibu ambayo yatatolewa tayari yamefanywa, lakini hakutoa maelezo zaidi.