Mapokezi ya Rais Samia Katika Uwanja wa Ndege wa KIA Akitokea Marekani Leo (Picha +Video)
Global Publishers April 28, 2022 0 Comments
SHARE THIS:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) wakati akitokea nchini Marekani tarehe 28 Aprili, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Aprili 28, 2022 amewasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) akitokea nchini Marekani amepokelewa na Makamu wa Rais Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM -Bara Ndugu Abdulrahman Kinana na Wananchi wa Arusha na Kilimanajaro.
Rais Samia akisalimiana na Makamu wa Rais Philip Isdor Mpango mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).Rais Samia akisalimiana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).Rais Samia akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM -Bara Ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya kuwasili uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) wakati akitokea nchini Marekani.Rais Samia akielekea kuwasalimia Wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro na Arusha waliofika kumpokea.Kikundi cha ngoma za asili cha Kimasai kikitoa burudani mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tarehe 28 Aprili, 2022.Rais Samia akiagana na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama mara baada ya kuwahutubia Wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro pamoja na Arusha katika uwanja wa Ndege wa KIA.