Rais Samia Ashiriki Uzinduzi wa Filamu ya The Royal Tour Arusha -(Picha +Video)
Global Publishers April 28, 2022 0 Comments
SHARE THIS:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi pamoja na wageni mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa Filamu ya Tanzania The Royal Tour uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Arusha International Conference Centre AICC Jijini Arusha tarehe 28, Aprili, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amesema kwamba wakati akiwa nchini Marekani kwenye uzinduzi wa filamu ya The Royal Tour, aliona kwenye mitandao watu wakimsema kwamba badala ya kufanya kazi yeye amejigeuza kuwa Rambo anaigiza.
Viongozi pamoja na wageni mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa Filamu ya Tanzania The Royal Tour uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Arusha International Conference Centre AICC Jijini Arusha tarehe 28, Aprili, 2022.
Kauli hiyo ameitoa hii leo Aprili 28, 2022, Jijini Arusha, wakati wa uzinduzi wa filamu ya The Royal Tour, yenye lengo la kuutangaza utalii na vivutio vya utalii vilivyomo hapa nchini.
“Nimetumia siku 8 nje ya ofisi, lakini wakati nafanya hili jambo kuna wanangu nikawa nasoma kwenye mitandao huyu Mama badala ya kufanya kazi huko amejigeuza Rambo, Schwarzenegger anafanya filamu huko anaigiza, lakini nikasema ngoja tuone kitakachotoka,” amesema Rais Samia
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwandishi wa Habari Maarufu wa Marekani ambaye ndiye mtayarishaji wa Filamu ya Tanzania The Royal Tour Peter Greenberg mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Mikutano wa Arusha International Conference Centre AICC Jijini Arusha kwa ajili ya uzinduzi wa Filamu hiyo tarehe 28, Aprili, 2022.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo ya Heshima kutoka kwa Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania Eliya Mjatta kuthamini mchango wake katika Tasnia hiyo mara baada ya uzinduzi wa Filamu ya Tanzania The Royal Tour Jijini Arusha 28, Aprili, 2022.