×

Anayedai Kuzaa na Ibraah Aibuka na Mazito, Adai Amemwachia Majukumu

Kim Mishepu akiwa na Ibrahim Nampunga almaarufu Ibraah.

Ibrahim Nampunga almaarufu Ibraah; ni staa mpya wa muziki nchini Tanzania ambaye kuna mwanadada anayejiita Kim Mishepu kwenye mitandao ya kijamii anayedai kuwa amezaa naye ambaye ameibuka na mambo mazito.

 

Kim Mishepu anadai kuwa Ibraah amepuuza majukumu yake ya uzazi licha ya kuwa walikuwa wameshiriki kikao na kuwa na makubaliano.

 

Mrembo huyo anadai kuwa, Ibraah amemwachia majukumu yote ya mtoto wao, jambo ambalo limekuwa changamoto kubwa kwake.

 

“Mtoto ni mdogo anahitaji matunzo. Mimi ni mwanamke ambaye anapambana. Kuna wakati siyo kwamba inabidi nishughulikie mtoto tu, niko na wadogo zangu ambao wananitegemea.

 

Mtoto wa Kim Mishepu ambaye baba yake ni Ibraah.

“Anavyokuwa ameniachia mimi nipambane kwa kila kitu inanipa ugumu sana. Kuna vitu vyangu vingi nashindwa kuvifanya sababu niko mwenyewe,” anasema Kim Mishepu.

 

Kim Mishepu anasema alipojitokeza kulalamika kwa mara ya kwanza takriban miezi minne iliyopita aliweza kushiriki kikao pamoja na Ibraah na mjomba wake na wakawa na maelewano.

 

Anasema kuwa, baada ya kikao hicho mjomba wa Ibraah alikuwa anafanikisha ushirikiano katika malezi ila baadaye akakatiza mawasiliano.

 

“Nilipoona hivo nikamtumia mwanasheria wangu. Mwanasheria wangu aliongea na meneja wa Ibraah, akaongea na Ibraah mwenyewe, lakini vitu vikawa haviendi poa,” anasema.

 

Mrembo huyo anasema kwa muda mrefu uhusiano wake na Ibraah haujawa mzuri na ndiyo maana mjomba wake alikuwa daraja kati yao.

 

Kim Mishepu anamshtumu Ibraah kwa kuwa na utoto mwingi huku akidai kuwa amekuwa akiogopa kuitwa baba.

“Labda ana utoto. Nimemzidi umri kwa mwaka mmoja. Nimezaliwa 1997 yeye amezaliwa 1998. Kitendo cha kuitwa baba amekuwa akikiogopa sana. Drama ni nyingi. Ibraah hamhudumii mtoto. Amekuwa mtu mgumu. Hata hivyo, ananiheshimu sana,” anasema Kim Mishepu.

 

Kim Mishepu anasema kuwa, yupo tayari kwa Ibraah kufanyia mtoto wake DNA ili kuthibitisha kuwa yeye ndiye baba mzazi.

 

“Ibraah naomba huduma za mtoto. Naomba tugawane sapoti. Nimechoka. Hata mimi ni binadamu, napambana. Kuna wakati napata na kuna wakati nakosa. Nimechoka kwa haya mambo yenu,” anasema.

 

Kim Mishepu anasema alianza mahusiano na Ibraah kabla hajawa staa na kumzalia mtoto mmoja wa kike aitwaye Yasreen.

Alipotafutwa Ibraah ili kujibu madai hayo hakuwa tayari kutoa ushirikiano hivyo jitihada zinaendelea.

Stori; Khadija Bakari, Dar

Leave a Comment