
RAIS Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, ametia saini Kitabu cha Maombolezo katika Ubalozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu Nchini, kufuatia kifo cha Hayati Sheikh Khalifa Bin Zayed Al Nahyan, Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu na mtawala wa Abu Dhabi.

Sheikh Khalifa Bin Zayed Al Nahyan alikuwa alifariki baada ya kuugua ugonjwa wa kupooza uliomfanya asionekane mbele ya macho ya watu kwa takribani zaidi ya miaka nane tangu mwaka 2014.
Mataifa mbalimbali ikiwemo Tanzania tayari yametuma salamu za rambirambi kwa Umoja wa Falme za Kiarabu, yakiongozwa na matafifa ya Misri, Bahrain Marekani pamoja na Tanzania.