×

Rais Samia Akiri Nidhamu Imeshuka Katika Utumishi wa Umma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema ni kweli nidhamu imeshuka  katika utumishi wa Umma na hiyo ni kwa sababu hakuna mafunzo katika kada mbalimbali za utumishi.

 

Rais Samia ameiagiza Tume ya Utumishi wa Umma kwenda kusimamia nidhamu ya Utumishi wa Umma kwani watumishi wengi wa Umma wanapanda vyeo bila kujua wajibu na majukumu yao kiasi kwamba utendaji kazi unakuwa mbovu.

 

Rais Samia amesisitiza kuwa watanzania wote wana haki sawa hivyo Tume ya Utumishi lazima ihakikishe kila mwenye sifa stahiki anakaa kwenye nafasi yake na si vinginevyo.

Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson alipata fursa ya kuongea wakati wa hafla ya kula kiapo kwa wateule mbalimbali

“Watumishi wa Umma wamejikulia tu, wanakwenda tu, wanapandishwa vyeo biula kupata mafunzo yoyote yale, naombamkalisimamie turudishe nidhamu kwenye utumishi wa Umma lakini uwajibikaji pia, juzi wamefurahi sana tumepanda madaraja kwa mserereko lakini huo mserereko maana yake nini hawajui mtu kapanda ngazi mbili tatu kwa pamoja lakini wajibu wake nini anakokwenda hajui, kwahiyo naomba mkasimamie hilo watumishi wetu hawajielewi nidhamu yao mpaka wapate vitisho.” Amesema Rais Samia.

 

Rais Samia amemaliza kwa kusisitiza Tume ya Utumishi inafanya kazi kwa kuzingatia miiko na maadili ya Utumishi wa Umma lakini pia kushirikiana katika kuhakikisha kuwa watumishi wa Umma wanafanya kazi kwa uadilifu bila kusubiri hadi watishiwe.

 

 

Leave a Comment