×

Yanga Yabanwa Mbavu na Biashara United, Mayele Atetema Tena

Kikosi cha Yanga kilichoanza dhidi ya Biashara United

KLABU ya Soka ya Yanga imeambulia matokeo ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Wanajeshi wa Mpakati Biashara United katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

 

Iliwachukua Yanga katika dakika ya 77 ya mchezo kupata bao la kuongoza kupitia kwa kinara wao wa mabao Fiston Kalala Mayele aliyetumia vizuri makosa ya walinzi na mlinda mlango wa Biashara United na kujiandikia bao lake la 14 katika msimamo wa Ligi Kuu ya NBC akiwa na mbao sawa na George Mpole wa Geita Gold.

Fiston Mayele mshambuliaji wa Yanga amefikisha jumla ya mabao 14 sawa na George Mpole wa Geita

Biashara United walipata bao la kusawazisha dakika mbili baadaye na hadi kipyenga cha mwisho cha Mwamuzi Ramadhan Kayoko kinapulizwa Biashara United 1-1 Yanga.

 

Baada ya mchezo huo Yanga wataendelea kubaki Jijini Mwanza kujiandaa na mchezo wa nusu fainali ya Kombe la FA dhidi ya watani wao wa Jadi Simba unaotarajiwa kuchezwa Mei 28 mwaka huu.

Leave a Comment