
Watu watatu wamefariki dunia kwa ajali iliyotokana na basi la Mohamed Classic linalotoka Arusha kwenda Mwanza kugongana na lori aina ya Fusso.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Benjamin Kuzaga amesema ajali huyo imetokea leo Jumanne Mei 24 huko Katesha wilayani Hanang’ Mkoani Manyara kwenye barabara ya Singida-Arusha.