
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Makamu M/Kiti wa Chama cha ACT – Wazalendo Zanzibar, Othman Masoud Othman, leo Mei 24, 2022 amekutana na kufanya mazungumzo na Wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Ngome ya Vijana wa Chama cha ACT-Wazalendo Taifa wakiongozwa na Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar, Ndugu Salim Bimani.

Kikao hicho kilichofanyika katika Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Migombani Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, kilijadili masuala mbalimbali yakiwemo yanayohusu maendeleo ya Vijana.M