×

Rais Mstaafu Dkt Jakaya Kikwete na Joachim Chissano Wakutana Pemba, Msumbiji

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais Mstaafu wa Msumbiji Joachim Chisano

RAIS Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa Msumbiji Joachim Chisano.

 

Dkt Kikwete akiwa nchini Msumbiji ameshiriki shughuli za Alliance for a Green Revolution in Africa (AGRA), Shirika linalojihusisha na mageuzi ya kilimo cha wakulima wadogo Barani Africa ambalo yeye ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi.

 

Vile vile Rais Mstaafu Dkt Kikwete alikuwa huko Msumbiji kwa  shughuli za jopo la wazee wa SADC (SADC Panel of Elders)  linalojishughulisha na kusuluhisha  migogoro na kuleta amani kwa nchi wanachama wa SADC ambapo yeye ni Mwenyekiti wake.

Leave a Comment