
HII leo Mei 24, 2022 Mshindi wa Tuzo ya Best Digital Journalist (Female) Anna Mbawala amekabidhiwa tuzo hiyo, Makao Makuu ya Global Publishers Sinza Mori Jijini Dar es salaam na waandaaji wa tuzo za Tanzania Digital Awards (TDA)
Tuzo za TDA zilikuwa na washiriki 278 katika vipengele mbalimbali ambapo kati yao walioibuka washindi ni 58 pekee.

Mchakato wa upatikanaji wa washindi ulifanyika kwa njia ya upigaji kura Mitandaoni zoezi lililofanyika kwa muda wa Mwezi mmoja.
Wakati huo huo Radio namba moja ya mtandaoni, +255 Global radio pia imekabidhiwa tuzo yao na TDA mara baada ya kuibuka kinara tena kwa mara nyingine katika kipengele cha Radio ya Mtandaoni ya Mwaka (Online Radio of The Year) ikimburuza Boresha Radio.