×

Kero ya Maji kwa Wakazi wa Kijiji cha Nega  B Wilayani Iringa Mbioni Kumalizika

Ukosefu wa maji katika kijiji cha Nega  B wilayani Iringa umesababisha wakazi wa eneo hilo kuoga maji pungufu katika familia zao ili kuwezesha kila mwanafamilia kupata japo ya kuoga.
Akizungumza Kwa niaba ya wananchi wenzake mkazi wa kijiji hicho Faraja Kagile amesema wanalazimika kufanya hivyo kutokana na uhaba wa maji uliopo kijijini hapo.
“Hapa kwetu tatizo la maji ni kubwa mno kwa hiyo ni lazima tuoge  maji kwa kijibana ili kila mwanafamilia aweze kupata ya kuoga”
Aidha amesema tatizo hilo lililodumu kwa miaka mingi liko mbioni kutoweka baada ya serikali kujenga mradi wa maji kupitia wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA).
Wananchi zaidi ya elfu tano kutoka vijiji vya Nega B na Ikengeza wilayani Iringa wanatarajia kunufaika na ujenzi wa mradi huo wa maji wenye thamani ya zaidi ya Sh Milion 540 fedha kutoka mpango wa maendeleo kwa taifa na mapambano dhidi ya Uvico-19.

Leave a Comment