×

Rais Samia Kupokea Kombe la Dunia la FIFA, Dkt Abbas Asema Taifa Limeheshimishwa

Dkt Hassan Abbas Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo

TANZANIA imechaguliwa kuwa miongoni mwa nchi chache za Afrika ambako Kombe halisi la Dunia la FIFA linalotolewaa kwa nchi zinazoshinda mashindano hayo, litapita.

 

Akiongea Dar es Salaam na waandishi wa habari leo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi, amesema litakapofika hapa nchini Mei 31, 2022, Kombe hilo litapokewa Airport na Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Mohammed Mchengerwa kisha litapelekwa Ikulu katika hafla ya mapokezi itakayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Dkt Hassan Abbas akiongea na waandishi wa habari

“Mbali na ujio wa Kombe la Dunia hili kwa hapa nchini ni tukio jingine kubwa la kimataifa la michezo kwa wiki hii tu Tanzania kuwa mwenyeji, juzi yameisha mashindano ya Nchi 10 za Afrika ya Baseball, leo yanakamilika mashindano ya nchi 7 za Afrika Mashariki ya Riadha U20 na U18 na leo tena Jumamosi pale Indoor Stadium mashindano ya nchi nne za Afrika ya ngumi za ridhaa yanaanza Uwanja wa ndani wa Benjamin Mkapa. Hii yote ni imani kwa Tanzania nchi yenye amani lakini pia Taifa la Royal Tour lenye vivutio vya kila aina,” alisema Dkt. Abbasi.

Leave a Comment