×

Swissport Yatangaza Gawio Kwa Wanahisa Wake la Sh. 29.8

Kampuni ya usafirishaji wa mizigo ya swissport imetangaza gawio kwa wanahisa wake la Shilingi 29.8 kwa hisa kwa mwaka 2021 ikiwa ni baada ya kampuni hiyo kupata faida ya Shilingi bilioni 2.1 sawa na asilimia 100 ikilinganishwa na asilimia sifuri ya mwaka 2020

Akizungumza katika mkutano mkuu wa wanahisa wa kampuni hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Mrisho Yassin amesema faida hiyo imetokana na kuimrika kwa biashara baada ya kupungua kwa makali ya uviko 19 duniani

Kwa mwaka 2020 kampuni hiyo ilipata hasara ya Shilingi bilioni 2.5 na ikashindwa kutoa gawio kwa wanahisa wake ambapo kwa sasa bei ya hisa moja ya kampuni hiyo inathamani ya Shilingi 1000.
Mkutano huo pia ulikwenda sambamba na uchaguzi wa wajumbe na mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa kampuni hiyo

Leave a Comment