×

Wydad Casablanca ya Morocco Yabeba Ubingwa Ligi ya Mabingwa Afrika -Video

 Wydad Casablanca ya Morocco wanafanikiwa kutwaa Ubingwa wa Club Bingwa Afrika kwa kuifunga 2-0 club ya Al Ahly ya Misri katika mchezo wa fainali uliyochezwa nchini Morocco.

Magoli ya dakika ya 15 na 48 yaliyofungwa na Zouhair El Moutaraji yameipa Wydad Casablanca ya Morocco ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wababe wa Misri, Al Ahly

Al Ahly waliokuwa wakitetea taji hilo, licha ya kushambulia muda mwingi katika mchezo huo wameshindwa kufurukuta katika fainali kwenye Uwanja wa Mohammed V Jijini Casablanca, Morocco

Ubingwa huo wa tatu kwa Wydad unawapa Dola 2,500,000 (Tsh. Bilioni 5.7) wakati Al Ahly wameambulia Dola 1,250,000 (Tsh. Bilioni 2.7) kwa kushika nafasi ya pili

Leave a Comment