×

Manara Afunguka Mazito Kuhusu Simba, Amtakia Kila Lakheri Pablo Franco

 

IKIWA ni dakika chache baada ya Klabu ya Simba kutangaza kuvunja mkataba na kocha wake mkuu, Pablo Franco, Raia wa Hispania, Msemaji wa Klabu ya Yanga ambao ni mahasimu wa Simba, Haji Manara amefunguka haya kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Kocha wa Simba Pablo Franco akiwa na Msemaji wa Yanga Haji Manara

“Kocha Bora mwenye nidhamu kubwa na mapenzi mazito na football pamoja na wachezaji wake anaondoka nchini. Pamoja na kufanya kazi katika Mazingiza magumu ya kukosa Proper Management iliyogubikwa na migogoro isiyoisha, Jamaa aliiwezesha Club yake kufika  Robo Fainali ya Shirikisho.

Msemaji wa Klabu ya Yanga Haji Manara

“Binafsi nitam-miss kwa uungwana wake na ucheshi wake. Kila la kheri rafiki yangu Pablo. Kwa msimu huu tu wewe ni Kocha wa pili kufukuzwa na naamini hadi msimu uishe tutasikia mengi. @pablofrancomartin,” amesema Manara

Leave a Comment