×

Nafasi za Kazi 8 MDAs & LGAs, Msaidizi Ustawi wa Jamii Daraja la II

POST MSAIDIZI USTAWI WA JAMII DARAJA LA II – 8 POST
EMPLOYER MDAs & LGAs
APPLICATION TIMELINE: 2022-05-28 2022-06-07
JOB SUMMARY N/A
DUTIES AND RESPONSIBILITIES i.Kutambua na kuhudumia watu walio katika makundi maalumu na mazingira hatarishi,

ii.Kuandaa mpango kazi wa mwaka kulingana na bajeti ya shughuli za ustawi wa jamii katika kituo cha kazi

iii.Kutambua na kufanya tathmini ya awali kwa watu wenye ulemavu, waathiriwa wa unyanyasaji wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto ili kuwaunganisha na huduma za ustawi wa jamii

iv.Kushiriki katika uainishaji wa mashauri mbalimbali yanayohusu ustawi wa jamii yasiyo ya kimahakama

v.Kupokea na kuandaa orodha ya mapendekezo ya msamaha wa matibabu na huduma nyingine za ustawi wa jamii kwa wanaostahili

vi.Kushiriki katika shughuli za ulinzi na usalama kwa mtoto

vii.Kushiriki katika shughuli za kuanzisha na kukagua vituo vya malezi na maendeleo ya watoto katika maeneo mbalimbali ikiwemo maeneo ya maafa na kambi za wakimbizi

viii.Kutambua na kushirikiana na wadau wa ustawi wa jamii na kuwaunganisha na watu wenye mahitaji maalum ili kupata huduma stahiki

ix.Kupokea na kukusanya takwimu kwa ajili ya kuandaa taarifa za wahudumiwa wa ustawi wa jamii

x.Kushiriki katika  ufuatiliaji wa mwenendo wa mashauri ya wahudumiwa wa ustawi wa jamii na kuandaa taarifa za uchunguzi wa kijamii wa awali na kuwasilisha katika ngazi husika ( Social Inquiry/ Investigation Report )

xi.Kutunza regista na kuhuisha kumbukumbu za wahudumiwa

xii.Kutoa elimu kwa jamii juu ya masuala mbalimbali ya ustawi wa jamii

xiii.Kufanya kazi nyingine yoyote atakayopangiwa na mkuu wake wa kazi kulingana na elimu na ujuzi wake

 

QUALIFICATION AND EXPERIENCE
  • Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne au sita na wenye mafunzo ya Stashahada katika fani zifuatazo; Social work, Sociology, Psychology, Social protection, Guidance and Counceling, Theology, Divinity, Child protection, Social policy, Early childhood development na Social gerontology

 

REMUNERATION TGS.C

BONYEZA HAPA KUTUMA MAOMBI

Leave a Comment