
BENKI KUU ya Dunia imeidhinisha kiasi cha Dola Bilioni 1.5 kama msaada kwa nchi ya Ukraine.
Hii ni sehemu ya msaada unaotolewa kwa ajili ya kulipa mishahara ya watendaji na wafanyakazi mbalimbali wa Serikali.
Msaada huu unaotoka Benki ya Dunia unfadhiriwa na mataifa ya Uingereza, Uholanzi, Lithuania na Latvia.
Zaidi ya kiasi cha Dola Bilioni 2 kilichoainishwa tayari kimeshatumwa Ukraine kama msaada.

Taarifa inasema kiasi hicho cha fedha kitasaidia Benki ya Dunia kutekeleza mipango yake mbalimbali ndani ya nchi ya Ukraine, kama vile Miradi ya Maji, Mazingira, Nishati, Barabara, Ulinzi, Elimu na Huduma za Afya.
Mnamo mwezi Aprili Waziri wa Fedha wa Ukraine alisema itagharimu zaidi ya Dola Bilioni 5 kila mwezi ili kuweza kukabiliana na hali ya mabadiliko ya uchumi wa nchi hiyo.