Polisi Yamsaka Raia wa China Zheng Lingyao Adaiwa Kuua Mtaa wa Kalenga, Ilala Dar
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamtafuta mtuhumiwa Zheng Lingyao (42), raia wa China mkazi wa Dar es salaam anayetuhumiwa kumuua Fu Nannan, (26), ambaye pia ni raia wa China.
Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo, Jumanne Muliro amesema tukio hilo limetokea Juni 11 saa 5:45 usiku katika mtaa wa Kalenga, Ilala ambapo marehemu alikuwa anaishi kwenye ghorofa ya tatu ya wapangaji.
“Mtuhumiwa anayetafutwa alifika eneo hilo na kumjeruhi kwa risasi tumboni mwanamke Nie Mnqin raia wa China na baada ya kumjeruhi alimfyatulia risasi Nannan na kufariki dunia,” amesema Muliro.