The House of Favourite Newspapers

CRDB Bank Pamoja Bonanza Lilivyofana Jijini Dodoma

0
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson akiongoza matembezi ikiwa ni sehemu ya Bonanza la Pamoja la Benki ya CRDB (CRDB Bank Pamoja Bonanza), yaliyoanzia kwenye viwanja vya Bunge na kuishia kwenye Uwanja wa Jamhuri na kufuatiwa na Michezo Mbalimbali ikiwemo ile ya Soka, Pete na Kikapu, jijini Dodoma Juni 25, 2022.

 

 

DODOMA 25 Juni 2022 – Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tulia Akson ameipongeza Benki ya CRDB kwa kuendelea kuandaa bonanza la pamoja la michezo lililopewa jina la “CRDB Bank Pamoja Bonanza” kwa mafanikiao makubwa pamoja na kuhamasisha utamaduni wa kushiriki katika michezo na kujenga afya na kuhamasisha mshikamano kwa Watanzania katika shughuli za maendeleo.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson (wa tatu kushoto) akiwa sambamba na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela pamoja na viongozi wengine wakiongoza mazoezi ya viungo muda mfupi baada ya kumaliza matembezi ‘CRDB Bank Pamoja Bonanza’, yaliyoanzia kwenye viwanja vya Bunge na kuishia kwenye Uwanja wa Jamhuri na kufuatiwa na Michezo Mbalimbli ikiwemo ile ya Soka, Mpira wa Pete, Kikapu nk.

 

 

Akizungumza katika bonanza hilo, Spika alisema kuwa bonanza hilo limeleta msisimko na mwamko mkubwa kulinganisha na miaka ya nyuma, ambapo mwaka huu idadi ya washiriki imeongezeka na kufanya maana na lengo halisi la mashindano hayo kupata umaarufu jijini Dodoma na Tanzania kwa ujumla.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson akizungumza katika Bonanza la Pamoja la Benki ya CRDB (CRDB Bank Pamoja Bonanza).

 

 

“Kwa mwaka huu tumeona hata ndugu zetu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar na pia vijana wetu wa Bongo Flava ambao kwa pamoja wameleta msisimko mkubwa na kuleta ushindani, hongereni sana ndungu zetu Bemki ya CRDB kwa kuwa na maono makubwa hivi”. Alisema Tulia.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson akimkabidhi kombe Nahodha wa Timu ya Bunge Sports Club, Mhe. Cosato Chumi baada ya kuibuka washindi wa jumla katika Bonanza la Pamoja la Benki ya CRDB (CRDB Bank Pamoja Bonanza), lililofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma Juni 25, 2022.

 

 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema Benki ya CRDB inaipa kipaumbele michezo, kwani michezo ni afya, inaleta umoja na upendo, inawaleta pamoja Wafanyakazi wa Benki na wadau mbalimbali wa Michezo nchini. Hivyo Benki inatumia bonanza hilo kama sehemu tu ya kuisogeza karibu na Serikali, Bunge na wadau mbalimbali nchini ili kupata nafasi ya kusikiliza mahitaji yaliyopo na kujua namna gani benki inaweza kushiriki katika mipango ya maendeleo ya nchi na kuthibitisha kauli mbiu yake ya “Ulipo Tupo” na kuwa ni benki inayomsikiliza Mteja.

Picha ya pamoja na Mabingwa wa CRDB Bank Pamoja Bonanza.

 

 

Naye Mwenyekiti wa Bodi wa Benki ya CRDB, Ally Laay aliwashukuru Wabunge na wadau mbalimbali wa serikali na wananchi waliohudhuria mashindano hayo na kujitokeza kwa wingi kushiriki bonanza hilo lililotanguliwa na matembezi yaliyo anzia katika viwanja vya bunge vikiwemo vikundi mbalimbali vya Jogging, wanafunzi wa vyuo na Sekondari pamoja na wananchi kwa kutambua umuhimu wa michezo.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson akimvisha medali, Mhe. Mama Salma Kikwete

 

Mashindano hayo yalimalizika kwa Timu za Bunge la Jamhuri wa Muungano kutwaa ushindi wa jumla kwa Mpira wa Miguu, Mpira wa Kikapu, Mpira wa Pete pamoja na Ule wa kuvuta kama (Tag of War) katika bonanza hilo.

Leave A Reply