×

Wakimbizi 46 Waripotiwa Kufariki Ndani ya Lori Lililotelekezwa Jijini Texas Marekani

Lori Lililotelekezwa na kusababisha vifo vya wakimbizi 46

JUMLA ya wakimbizi 46 wamekutwa wamefariki ndani ya Lori ambalo lilikuwa limetelekezwa nje kidogo ya jiji la Texas Marekani huku zaidi ya wengine 16 wakiwemo watoto 4 wakiwa mahututi na kupelekwa hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

 

Taarifa zinadai kuwa miili ya manusura ilikuwa ya moto na kutokana na kuathiriwa kwa joto kali lililosababisha vifo vya wengine 46.

 

Watu wanaofanya biashara za kusafirisha watu mara nyingi hutumia Malori kwa ajili ya kuwasafirisha wakimbizi wasio na vibali mara tu wanapofanikiwa kuingia ndani ya nchi ya Marekani.

 

Naye Meya wa Mji wa San Antonio, Texas Ron Nirenberg amenukuliwa akisema:

Polisi wa zimamoto walifika eneo la tukio na kutoia msaada kwa manusura

“Walikuwa na watoto nadhani walikuja kwa ajili ya kutafuta maisha mazuri, ni janga kubwa sana na la kutisha kwa binadamu.”

 

Mkuu wa kitengo cha zimamoto katika Mji huo Charles Hood amesema:

 

“Hatutakiwi kufungua Lori na kuangalia miili iliyogandamana humo, wote sisi tumekuja kufanyakazi pasipo kutegemea kuona hiki tulichokiona.”

 

Lakini pia aliongeza kwa kusema kuwa Lori hilo lililokuwa limetelekezwa halikuwa na huduma ya hewa wala huduma ya maji.

 

 

 

Leave a Comment