×

Dereva Afunguka Gharama za Kukodi Gari la Ubingwa la Yanga

Dereva wa basi la ubingwa wa Yanga

YANGA wametisha sana! Hivyo ndivyo unavyoweza kusema. Moja kati ya vivutio katika sherehe za Ubingwa wa Klabu ya Yanga ni pamoja na basi la wazi ambalo wamelikodi kutokea Uganda kuja nchini Tanzania katika parade ya Ubingwa.

 

Sasa kutokana na tukio hilo la aina yake, watu wengi wamekua wakihoji na kutamani kujua gharama za kuleta basi hilo nchini kwa siku ni kiasi gani.

 

Dereva wa basi hilo ameweka wazi kuwa, kwa makadirio, kukodi basi hilo ni kiasi cha dola za Marekani 1,000 (Tsh milioni 2.3) kwa siku.

Basi lililotumika na klabu ya Yanga kwa ajili ya sherehe za ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2021/2022

Dereva huyo amesema basi hilo kwa Uganda limekuwa likitumika kwa ajili ya kufanya tour za mjini na za shule, sherehe mbali mbali zikiwemo harusi, za kuzaliwa na hata mikutano vyote vinafanyika ndani ya basi.

Yanga imepokea pongezi kutoka kwa watu maarufu katika tasnia soka akiwemo koca mwenye mafanikio makubwa barani Afrika raia wa Afrika Kusini Pitso Mosimane

Dereva huyo amefafanua kuwa aliwahi kuja Tanzania kama abiria, lakini kuja na gari hiyo kwa shughuli hizo za mpira kwake ni mara ya kwanza na kwamba jambo hilo ni zuri sana na hajawahi kuona kwao Uganda.

 

“Ni jambo zuri sana, aina ya mashabiki na sapoti wanayotoa kwa timu kama hivi, sijawahi kuona,” alisema dereva huyo.

Leave a Comment