Manchester United ilivyoichakaza Swansea 2-1
Kiungo wa Man United, Juan Mata akipiga shuti mbele ya beki wa Swansea katika mchezo uliopigwa jana kwenye Uwanja wa Old Trafford na United kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Leon Britton (kushoto) akichuana na nahodha wa United, Wayne Rooney.
Kipa wa Swansea, Lucas Fabianski akijaribu kuokoa mpira uliozama wavuni baada ya kazi nzuri ya straika wa United, Antony Martial.
Martial akishangilia baada ya kuipatia United bao la kwanza kwenye dakika ya 47.
Wachezaji wa United wakipongezana baada ya kutangulia kwa bao 1-0 lililowekwa na Martial.
Rooney alionekana kuwa kwenye ubora wake usiku wa jana na alifanikiwa kuipatia bao la pili timu yake dakika ya 77.
Rooney akishangilia kwa aina yake baada ya kuwahakikishia pointi tatu muhimu Mashetani Wekundu.
Rooney katika purukushani za kuwania kufunga dhidi ya mabeki wa Swansea.
Gylfi Sigurdsson (kushoto) akipiga kichwa safi mbele ya Mata (aliyeruka juu) na kuipatia Swansea bao la kufutia machozi.
Sigurdsson akishangilia baada ya kutupia bao dakika ya 70.