Vodacom Tanzania Yakabidhi Vifaa kwa Shule ya Wasichana Yatima
VODACOM Tanzania Foundation leo imekabidhi vifaa na samani kwa Shule ya Wasichana ya Bethsaida mjini Dar es Salaam ambavyo kampuni ilishinda katika mashindano ya makampuni ya Vodacom duniani.
Akiongea wakati wa makabidhiano, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Vodacom Tanzania, Vivienne Penessis alisema, “Elimu ni msingi pekee ambao unampatia mtu kianzio cha kujenga maisha bora. Hii ni kweli zaidi kwa Watoto yatima ambao tegemeo lao ni elimu pekee.”
Shule ya Wasichana ya Bethsaida ilichaguliwa kupokea msaada huu kwakuwa ni moja ya shule chache zinazotoa elimu ya sekondari kwa Watoto yatima wa kike nchini.
Mkurugenzi wa Vodacom pamoja na wafanyakazi wengine wa kampuni waliikabidhi shule hiyo viti 100, vitabu Zaidi ya 300 pamoja na vifaa 20 vya kuzalisha umeme wa jua. Bipenessis alielezea Imani yake kuwa msaada huo utatumika ipasavyo kwani kampuni ya Vodacom ilijiridhisha juu ya utaalam na moyo wa kujitoa kwa wafanyakazi wa shule ya Bethsaida.
Msaada huu unaendana na malengoya Vodacom Tanzania kuongeza ujumuishwaji katika elimu. Hivi karibuni, kampuni ya Vodacom ilizindua mpango wa kupanua wigo wa mfumo wa E-Fahamu kufikia nchi nzima. E-Fahamu ni huduma inayotoa mawaidha ya elimu yenye viwango vya kimataifa na vyenye kukidhi miongozo ya serikali juu ya elimu.
Kuhusu Vodacom Tanzania Foundation
The Vodacom Tanzania Foundation ni sehemu ya kampuni ya Vodacom Tanzania PLC yenye mamlaka ya kutoa huduma za kijamii zikiwa zinawalenga zaidi wanawake na vijana.
Foundation inajumuisha utoaji wa hisani na kutumia uwezo utokanao na teknolojia kuleta suluhisho kwa mahitaji ya kijamii. Ikishirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali, Vodacom Tanzania Foundation imesaidia zaidi ya miradi 120 hadi sasa ikiwa imewekeza zaidi ya shilingi bilioni 15 kuboresha maisha ya watanzania.