
MUME wa Msanii na Mtangazaji wa Wasafi Media Diva the Bawse Lady, anayefahamika kwa jina la Abdulrazack amesema kwa mtangazaji huyo alifuata uzuri wake ambao unachagizwa na utamu wake lakini pia sauti yake nzuri inayotekenya.
“Ni mwanamke mzuri ana macho mazuri, shape nzuri anaongea vizuri ana sauti tamu, sauti inatekenya kwahiyo nikaona mimi nataka kutekenyeka nikamvuta. Eeeh niliangalia hayo mengine sikuyapa nafasi.” Amesema Abdulrazack
Kwa upande mwingine Abdulrazack amebainisha kuwa anatongozwa sana na wanawake mbalimbali kila siku wengi wao wakiomba kuzaa naye na wengine ni watu maarufu pamoja na watu wakubwa wa Serikalini.

Abdulrazack amesema hayo katika mahojiano yake na Global TV pamoja na Global Radio ambapo pia amebainisha kuwa amekuwa akishangazwa na watu wanaodai kwa Diva alifuata umaarufu wake na siyo mapenzi lakini yeye amethibitisha kuwa mahusiano yake na Diva hayahusiani na umaarufu wake kwani hata yeye pia ni maarufu kupitia kazi yake anayoifanya ya ushauri wa masuala ya mahusiano na mapenzi.
Aidha Abdulrazack amekanusha habari zilizoenea katika mitandao ya kijamii kuwa Diva alikunywa sumu kwa kubainisha kuwa Diva hakunywa sumu bali aliharibikiwa ujauzito wake kitendo ambacho kilimvunja moyo na kumfanya kuondoka katika eneo la hospitali alipokuwa akipatiwa matibabu kutokana na sababu kuwa alishindwa kuvumilia kupokea taarifa za kuharibika kwa ujauzito wa mke wake.