
IMEFICHUKA kuwa Bilionea namba moja duniani, Elon Musk ambaye ni mmiliki wa Kampuni ya Tesla na SpaceX alipata watoto mapacha mwaka jana na Ofisa Mkuu katika moja ya kampuni zake, mtandao wa Insider umeripoti.
Mama wa watoto hao, Shivon Zilis mwenye umri wa miaka 36 kutoka Canada ni Afisa Mkuu wa Kampuni ya Neuralink inayomilikiwa na Elon, na amefanya kazi katika kampuni zake nyingi, zikiwemo OpenAI na Tesla.
Musk, ambaye Mei 24, 2022 aliposti katika mtandao wake wa Tiwtter akiandika kuwa; “Idadi ya watoto wanaozaliwa nchini Marekani imekuwa chini ya kiwango kwa miaka 50” na ali-pin Tweet hiyo ambayo ilisomwa na watu Zaidi ya milioni 100 wakimpongeza kwa kupata watoto na mwanamama Shivon Zilis.
Imebainika kuwa, kuna nyaraka za mahakama ambazo zimenaswa Musk akibadilisha majina ya watoto hao ili kufananisha na majina yake ya mwisho na jina la mama yao.
CNN Business imesema lakini haijathibitisha kuwa moja ya nyaraka hizo zinaonyesha Musk alizijaza Aprili 2022 na kufanikiwa kubadilisha mnamo Mei 2022 ambapo tarehe na saini ya Musk kwenye nyaraka hizo.